Kuna jamaa mmoja Mchaga alikufa, akahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Kuna jamaa mwingine akawa anapita chumbani hapo, kwa bahati mbaya akadondosha ufunguo wake. Marehemu Mchaga aliposikia sauti ya ufunguo kudondoka...akazani hela, akafufuka na kuuliza; hizo ni hela?
Jamaa akajibu; hapana ni ufunguo. Marehemu Mchaga akafa tena.
2 comments:
Asante kweli msee wangu na ujumbe wako umetufikia wadau wako!
==========================
KARIBU KWETU KILIMANJARO [CHAGGALAND]
Huu ndiyo mpangilio unaowatofautisha Wachagga kwa msingi wa maeneo yao:-
Wasiha
Wamachame
Wamasama
Wakindi
Wakibosho
Wauru
Waoldmoshi
Wambokomu
Wakirua
Wakilema
Wamarangu
Wamamba
Wamwika
Wakeni
Wamkuu
Wamashati
Wasseri
Wangasa
FURAHIA MAJINA YA MAENEO YA KWETU
===================================
Wazungu walipofika kwetu na kuona kilele cha kibo walisema 'that is kibo alone' na waliosikia wakatamka 'KIBORILONI'.
Wakaweka kibao kinachosomeka' check train' na wenyeji wakasoma 'CHEKERENI'.
Walipofika kwenye sherehe wakaona mbuzi ameokwa vizuri wakasema 'this is wonderfull' wenyeji wakasema 'NDAFU'.
Walipoona njia inayotoka mnadani kwenda kiwanda cha nyama wakasema 'cow way' waliosikia wakasema 'KAWE''
Walipouliza hapa ni wapi wakajibiwa ni 'kwa Musa Hasan' wakasema 'MSASANI'
Waliposikia wenyeji wakisema 'mambo sasa' wakasema 'MAMBASA' na wenzao waksema 'MOMBASA'
Haya ndiyo baadhi ya majina ya kwetu na wala usishangae. Iwapo katika maktaba yako umehifadhi baadhi ya majina ya kwenu tafadhali yaweke hadharani ili wadau wacheke kabla ya kutabasamu.
Post a Comment