Wednesday, September 21, 2011

MAISHA UPANDE WA PILI WA SARAFU - BY LADY JAYDEE!

Huku hakuna hali ya msongamano kama mjini, hakuna joto kama mjini....ni baiskeli tu tena wala sio nyingi kama magari ya mjini. Ajali si mara kwa mara, labda iwe ya kuumwa na nyoka shambani au kuanguka toka juu ya mti au kutumbukia kisimani wakati unateka maji, huhitaji steel wire kusugulia hizo sufuria zinazoonekana ziking'aa hapo juu ya kichanja......unahitaji mchanga laini tu! ambao huundwa kama kichuguu na wadudu wanaojenga maskani yao pembeni mwa nyumba wanaojulikana kama fukufuku.
Hapo kilichogharimu ni hayo masufuria tu! ila hiyo miti iliyotumika kutengenezea kichanja ni bure.

- By Lady Jaydee.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Safi sana.....maisha ya kijijini..

WATEMBELEAJI