Ee Mungu wangu mpendwa sana....uniokoe, unisaidie hima; dunia na mambo yake yote yananisonga sana, na mwovu ananisukuma; kulia, kushoto, mbele na nyuma.
Kimbilio langu wewe Mungu wangu, ingawa mimi ni mdhambi...wewe ni mwingi wa huruma, wewe ndiwe pekee mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira kwangu kwa mambo nikukoseayo. Mungu wangu mpendwa wangu nisaidie yule mwovu niepushie kabisa! wewe nikutumikie milele na milelel. Neno lako liwe taa kwangu ya kuniangazia...nifute giza la uovu na dhambi. Dunia ina mazuri mengi yanivuta, hakika yananidanganya sana ili nikusahau wewe Mungu wangu mpendwa wangu na muumba wangu. Nami ninasema siwezi kabisa kuku kana kamwe!
No comments:
Post a Comment