Sunday, September 18, 2011

TAFAKARI YANGU YA JUMAPILI HII!

Ee Mungu wangu, umenichunguza mimi ukanifahamu nilivyo, wayafahamu matendo yangu; nikitembea au nikisimama, nikaapo, nilalapo, niamkapo....kila kitu nifanyacho wewe unanijua mimi jinsi nilivyo.
Nikiwa kazini wanijua na kuniepusha na hatari mbalimbali, wewe wayajua mawazo yangu ningalipo bado nafikiria....wewe tayari wayajua, nikifanya mabaya gizani wewe unanijua tu na kunisamehe.

Wanizunguka kila upande na kuniwekea mkono wako mwenye baraka tele, bila wewe Mungu wangu mimi si kitu kabisa!
Nikimbie wapi mbali nawe, niende wapi nikajifiche wewe unanijua tu! nikipanda juu wewe upo, nikijilaza chini kuzimu wewe unanijua mimi. Umeniumba mwili na roho ulinitengeneza tumboni mwa mama yangu, hata kabla sijazaliwa wewe ulinijua mimi na kunithamini, uwezo wako ni wa ajabu sana ee Mungu wangu.

Ee Mungu wangu mwema mno nakushukuru sana tena sana kwa mema mengi sana unayo nijalia kila siku za maisha yangu, bila wewe mimi si kitu kabisa.

- Asante sana Mungu wangu kwa kunipa haya maisha!

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Baraka sala nzuri sana nimeipenda na najua Mwenyezi Mungu ameikubali na amekusikia maombi yako.JUMAPILI NJEMA NAWE na aheant sana kwa tafakari hii.

Anonymous said...

kweli Yasinta ni sala nzuri sana, hongera.

Baraka Chibiriti said...

Asante sana Dada Yasinta!

WATEMBELEAJI