.........DHIDI YA BAA LA UJINGA, UMASKINI NA MARADHI DUNIANI.
Ulimwengu wa Utandawazi unaendelea kukumbana na kinzani pamoja na mmong'onyoko wa tunu bora za kimaadili na kiutu, hali ambayo imekuwa ikichambuliwa kwa ufasaha mkubwa hasa katika hali yake ya ukweli katika upendo.
Tunafahamu fika changamoto inayoendelea kutolewa na Shirika la chakula na kilimo la umoja wa Mataifa; FAO.....kwamba halina fedha za kutosha kusaidia mamilioni ya watu wanaokabiliwa na uhaba wa chakula na utapiamlo. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba; Serikali nyingi zimediriki kutoa mamilioni ya fedha kwaajili ya kuyakingia kifua Mabenki na taasisi za fedha zilizokuwa zinaelekea kufilisika kutokana na myumbo wa uchumi Kimataifa.
Kiasi cha fedha kilichotengwa katika kipindi cha muda mfupi tu kingeweza kufuta baa la umaskini duniani, kama fedha hizo zingeelekezwa katika mkakati huu. Yote haya yanaonesha kwamba; licha ya mikakati inayotolewa na Jumuiya ya Kimataifa, lakini bado kunakosekana ule utashi wa Kisiasa wa kumwilisha maazimio haya katika uhalisi wa maisha na malengo yake yanayodai uwajibikaji fungamanishi.
Kumekuwepo na ubadhirifu wa mali ya Umma na ufisadi unaofanywa katika masuala ya kisiasa, kiasi kwamba baadhi ya wachunguzi wa masuala ya Kijamii wanadhani kwamba; siasa kimekuwa ni kichaka cha baadhi ya watu kujitafutia umaarufu katika medani za kisiasa, utajiri wa haraka haraka...kiasi kwamba wanasahau kuwa wajibu wao kwanza ni kwaajili ya mafao ya wengi na huduma kwa Jamii katika mapambano dhidi ya baa la Njaa, Umaskini, Magonjwa na Ujinga.
Kuna haja ya kutoa kipaumbele cha kwanza kabisa katika Utawala wa sheria, maadili mema ya uongozi na mafao ya wengi, kama sehemu ya mchakato wa kujenga Jamii inayojikita katika misingi ya haki, amani, upendo na mshikamano wa dhati.
Licha ya madhulumu na kejeli kutoka kwa wanasiasa waliofilisika kisiasa na kiutu, wanaojali masilahi yao binafsi, mshikamano wa pamoja katika kutolea shuhuda za msingi; Utu na Maadili mema, ni kilio cha watu wengi wa nyakati hizi. Ili kujenga utamaduni wa haki, amani na utulivu.....hizi ni nyenzo msingi katika mapambano dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi.
Hakuna maendeleo endelevu....pasipo na amani, kwani amani ndilo jina jipya la maendeleo kwa mwanadamu. Huwezi kupambana na umaskini kwa kukumbatia utamaduni wa kifo kwa kudhani kwamba; ongezeko la idadi ya watu ndicho chanzo kikuu kinachowatumbukiza watu wengi katika umaskini. Rasilimali watu inahitajika ili kufanikisha maendeleo endelevu ya binadamu.
Watu wanahitaji msaada unaoheshimu Utu wao kama binadamu na kamwe si msaada unaotaka kuficha Utu na Heshima yao kama Binadamu. Watu wanataka maendeleo na wala si vibaraka kwa mawakala wa misaada kutoka Jumuiya ya Kimataifa kwaajili ya mafao yao binafsi. Hii ni changamoto endelevu ninayoiwaza mimi.....katika maisha ya Jamii zetu!
No comments:
Post a Comment