Thursday, October 27, 2011

LEO NDIO SIKU YA MAZISHI YA KIJANA MARCO SIMONCELLI aka SIC.

Champion wa Moto Gp, mwendesha pikipiki za mashindano ya Kimataifa, Marco Simoncelli, aka SIC....amezikwa leo, baada ya kupata ajali Jumapili iliyopita huko nchini Malesia. Mimi nilifuatilia misa ya mazishi yake kwenye TV, ambayo yalifanyika huko Coriano-Rimini, jirani sana na hapa ninapoishi. Misa takatifu iliendeshwa na Mhashamu Askofu wa Jimbo la Rimini. Kwakweli watu walikuwa wengi sana...nilijikuta machozi yakinidodoka tu, nilijaribu kujizuia lakini wapi....kijana mdogo wa miaka 24, alikuwa simpo sana kwa watu mwenye kucheka daima na kuchekesha kwa sana.

- Kwaheri Marco Simoncelli aka SIC, Mungu akupe pumziko la milele...amina!



No comments:

WATEMBELEAJI