Saturday, October 29, 2011

MKUU MICHUZI; HONGERA KUSIMAMA KWA SOKOINE!

Hii picha ni ya muda mfupi uliopita nimeipenda sana, ya Mkuu Michuzi akiwa katika Kijiji cha Wami-Sokoine. Ni barabara kuu ya Morogoro - Dodoma. Kwakweli hii barabara nimeipita sijui mara ngapi...hata siwezi kuhesabu, maana ni barabara inayonipeleka nyumbani kwetu Dodoma, lazima niipite tu hata iweje....labda nipande ndege, hapo ndipo sita ipita. Nami uwezo wa kupanda ndege kutoka Dar - Dom, sina. Sijawahi kuona gari la kiongozi yoyote limesimama maeneo haya kutoa heshima kwa aliyekuwa kiongozi wetu Mkuu kabisa, alikuwa na heshima kubwa sana katika Taifa letu....lakini hola, tena kila siku nipitapo njia hii lazima nikutane na mashangingi ya Mawaziri, wabunge na viongozi mbalimbali wa Taifa hili....maana barabara hii ni muhimu sana inayowapeleka mpaka Bungeni na makao Makuu, lakini sijawahi kukuta shangingi limepaki hata siku moja, nami barabara hii naipita sana. Ambao hawajui hii ni sehemu muhimu sana....alipopata ajali Waziri wetu Mkuu Edward Moringe Sokoine, ni km 40 kutoka Morogoro mjini, ukielekea Dodoma....yeye alikuwa ametoka Dodoma anaenda Dar ndipo mauti yalipo mkuta sehemu hii. Sasa ni kijiji cha Wamasai...Masai wengi sana katika kumuenzi Baba huyu Sokoine, mmasai mwenzao. Ni kijiji kinaitwa Wami-Sokoine. Hivi kweli viongozi wetu hawaoni umuhimu wowote kuhusu swala hili? au ndo zarau tu? Huyo baba Sokoine alijitoa maisha yake kututumikia sisi....je sisi tunamuenzi vipi? Yaani hapa palikuwa pameisha sana tena sana...watu walilalamika sana, kidogo wamepakarabati sasa. Mimi binafsi ningependa paheshimike sana...lakini ndo hivyo tena. Jamani jamani...hivi neema tutapateje kama tunapuuzia mambo kama haya....hata Mwalimu Nyerere mwenyewe bado kabisa hatumwenzi ipasavyo. Hivi Watanzania wangapi mpaka sasa wamefika Butiama kwa Mwalimu kutoa hata shada la maua tu! Niliongea na Mtoto wa Mwalimu; alikuwa ananiambia ni watu wachache sana tena sana wanaofika kutoa heshima kwenye kaburi la Mwalimu, visingizio vingi watu hawana uwezo; wakati baa kila siku zinafurika....hivi kweli ni haki?

- Mimi binafsi nimemsifu sana mkuu Issa Michuzi, kusimama na kutoa heshima yake kwa Waziri wetu Mkuu, maana mimi bado namwita Waziri Mkuu kwa heshima yake na mchango wake mkubwa kwa nchi yetu. Watanzania tubadilike jamani.

No comments:

WATEMBELEAJI