Wednesday, October 26, 2011

NIMEPATA UJUMBE HUU........KUTOKA KWA BABA ROSTAM!

Siku ya Ijumaa tarehe 07/10/2011, mke wangu alijifungua mtoto wa kiume....na tulikubaliana amchagulie jina yeye mtoto, sasa usiku huo nikiwa narudi home toka kwenye mishemishe zangu, mke wangu ananiambia kampa jina mtoto la ROSTAM....nikadhani ananitania kumbe She's serious, na yeye anajua kabisa tena vilivyo msimamo wangu dhidi ya mafisadi...lakini yeye kasisitiza kuwa hajachagua jina hilo ili kunichokoza bali analipenda tu jina hilo. Licha ya kuwa mtu maarufu mwenye jina kama hilo hapa TZ anahusishwa na tuhuma za rushwa, kwa kuwa tulikubaliana awali kuwa yeye ndo atampa jina mtoto....sina jinsi imebidi nikubali kuwa; BABA ROSTAM kuanzia leo hii, je ungekuwa wewe ungeamuaje?

- Nami nasema; Pole sana BABA ROSTAM aka (Baba Fisadi), lakini ni jina tu lisikupe shida sana....

No comments:

WATEMBELEAJI