Sunday, October 16, 2011

TAFAKARI YANGU KATIKA JUMAPILI HII NJEMA.

Nimeishika njia ya kunipeleka Mbinguni.....ni Yesu wa Nathaleti, njia kweli na uzima! Amejifungua kwangu nami nimemkubali kabisa; katika shida zangu namkumbatia Yesu wangu, katika tabu zangu namkumbatia Yesu wangu, katika raha zangu namkumbatia yeye tu! Hata kama ninalia namkumbatia yeye tu, hata kama ninacheka namkumbatia Yesu wangu....yeye ni Bwana na Mwokozi wangu.

Matatizo yaliponikabili mimi...nililia na nilisahau na kuipoteza njia, na tatizo kubwa lilikuwa utajili nilisema sikubali kufa maskini; lakini niliyo yakuta huko kwenye utajili yalinishinda kabisa.....eti nimtoe mwanangu kafara, kwanini? Nikasema siwezi kabisa, na nikasema kwa sauti kubwa; ya dunia siyawezi kabisa....ila namkumbatia Yesu wangu mwema!

Injili ya Bwana inazidi kuhubiliwa, nayo makanisa yanazidi kuongezeka...hapo mimi ninasema; asante sana Yesu! Tatizo lipo kwa wahubiri, hivi kwanini wahubiri mnarumbana? na kusema makanisa mengine hayana wokovu, mnagombania waamini, kwanini? kwaajili ya mapato? Niacheni mimi makanisa siyawezi kabisa....bali namkumbatia Yesu wangu mwema.

Wewe shetani niache kabisa...mimi nimempokea Yesu tu! Bwana na Mwokozi wangu; utapeli sitaki tena, ujambazi sitaki tena, uchawi sitaki tena.......matunguli yako chukua nenda zako, na hirizi zako chukua nenda zako kabisa, kawape wengine wasio mjua Yesu.

No comments:

WATEMBELEAJI