Friday, October 7, 2011

TIMIZA WAJIBU WAKO......

Ee ndugu, timiza wajibu wako popote pale unapoihudumia Jamii.....ukiwa kiongozi au msanii, matendo yako yalingane na unachosema. Kiongozi wa Serikali au kiongozi wa Jamii utambue macho ya watu wote yapo kwako wewe, ukiwa msanii, mwimbaji au mwigizaji utambue kuwa wewe ni kioo cha Jamii. Mlei, mwanakwaya, Katekista au Kasisi....utambue macho ya watu wote yapo kwako wewe, nawe unayesikia maneno haya popote pale ulipo.... Jamii yakutazama utambue nawe ni kioo cha Jamii.
Tukisema Kiongozi, mtu yoyote yule ni Kiongozi, katika nafasi yako ile ambayo upo; wajibika vizuri, acha ufisadi na dhuruma na upendeleo....uwe ni mwiko kwako. Amani ikutawale kiongozi uwajibike vizuri, usisubiri wakati wa uchaguzi tu! kwa maana ipo siku watu watakuchoka tu, kwa maneno yasiyo na utekelezaji.
Kama msanii unaimba au kuigiza matendo yako nayo yawe mfano, kama ni kiongozi wa dini uchunge kondoo wako vyema. Ndugu rekebisha mapungufu yako kama yanayo athari kwa Jamii, naye Mungu atakubariki......Mungu atanyoosha mapito yako.

No comments:

WATEMBELEAJI