Monday, October 17, 2011

WATOTO YATIMA WA MAKALALA.WAKIFURAHIA KUPATA MCHEZO MPYA!



Watoto yatima wa Kituo cha Makalala - Mafinga - Iringa, wakifurahi sana kupata mchezo mpya. Nakumbuka siku tulipo wapelekea mchezo huu....walikataa hata kwenda kula chakula cha mchana kwa furaha waliokuwa nayo kwa kupata zawadi kama hii, yaani niliona watoto wanavyofurahi mpaka nilitokwa na machozi kwa mbali.

Huwa najiuliza sana, kuna vitu vingi sana na mambo mengi sana tunatumia hela vibaya sana hata hatukumbuki kabisa kusaidia wanaohitaji msaada, tena wakati mwingine ni kwa jambo ndogo tu kama hili la mchezo huu....unasababisha watoto wanapata furaha isiyo na kifani. Hela ngapi tunatumia kwenye anasa tu! Lakini watoto wengi sana wanahitaji msaada na hasa kuimarisha maisha yao ya hapo baadae. Huwa najilaumu sana hata mimi mwenyewe binafsi kabisa, kwa kutumia hela wakati mwingine bila kufikiri vizuri....ambapo inaweza kuwasababishia wengine furaha sana tena sana katika siku yao, au mwezi mzima. Fikiri ndugu mdau kwa kidogo ulicho nacho na ugawane na mwezio mwenye shida sana kuliko wewe!



No comments:

WATEMBELEAJI