Basi la Kampuni ya Budget....likiwa limepinduka eneo la Mlimanyoka Jijini Mbeya hapo jana. Abiria 50 wamenusurika katika ajali hiyo, majeruhi walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya, ambapo hali zao zinaendelea vizuri.
Dereva wa basi hilo aliyejulikana kwa jina moja la Bwana Mwamtobe, alikuwa akijaribu kuyakwepa malori mawili yaliyokuwa yakipandisha katika Mlimanyoka maeneo ya Uyole Jijini Mbeya, ndipo alipoangusha basi hilo.
- Picha na Habari kwa hisani ya Mbeya yetu.
No comments:
Post a Comment