Thursday, November 17, 2011

MKUU KALINGA NA KISIMA CHA MAJI....TUNZA MAJI...MAJI NI UHAI.




Safi sana hii kutoka kwa Kalinga, anayeishi huko USA...akiwa likizo huko Changalawe - Makalala B - Mafinga - Iringa, na kujitolea kwa kuchimba kisima. Shida ya maji Kijijini sasa mambo safiii....ni mfano mzuri sana wa kuigwa kwetu sisi sote tukiwa nje ya nchi, kama huko tuliko mambo mazuri huna budi kukumbuka na wenye shida, hasa vijijini mwetu kwenye shida sana kama hizi za maji nk. Ukiwa Majuu a.k.a Ugaibuni basi unajipendelea wewe tu na kusahau kabisa ulikotoka hii siyo nzuri....hivyo kama una uwezekano saidia na wenzako wenye shida.


- Hongera sana Kalinga, Mungu atakuzidishia zaidi na zaidi kile ulichopunguza kusaidia Jamii yetu. Na asante sana kwa upendo wako wa dhati kwa wenzako.


No comments:

WATEMBELEAJI