Pichani ni moja ya Kijana mkazi wa Kijiji cha Kipera, ambaye mbali na kulima zao hili anasema; ''msimu ukifika ni ajira kwa kila mtu Kijijini hapo alimaye na asiyelima nyanya. Anasimulia kuwa wapo ambao hujishughulisha na uvunaji wa nyanya mashambani, usombaji kutoka shambani hadi vilinge vya wafanyabiashara, upangaji katika matenga...kama afanyavyo yeye na upakiaji katika magari.'' Pia anasema wapo wanaofanya kazi ya kukata majani kwaajili ya kupangia nyanya hizo katika matenga. Anasema; msimu wa mavuno ya nyanya wafanyabiashara wengi sana hufika Kijijini hapo hivyo akina mama na watu mbalimbali hufungua migahawa ya chakula na kufanya pato la wakazi wa Kijiji hicho kukua kipindi hicho. Lakini analia na bei ambayo mkulima hupata, ambapo tenga moja la kuingia plastiki 3 za lita 20 hununuliwa kwa kati ya Tsh.5000 na 8000/= kulingana na ubora wa nyanya ulizonazo. Ipo haja ya Serikali kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi wa Kiwanda cha kusindika nyanya Kijijini hapo ili kukuza kipato cha wakazi wa Kijiji cha Kipera.
No comments:
Post a Comment