Ninafurahi sana kuwa nawe Yesu, Bwana wangu nakupenda sana! Pendo lako kwangu ni la ajabu sana, pendo kuu lenye utukufu! nimefurahi sana kuwa nawe Bwana.
Najitoa kwako Bwana nipokee, nifundishe kukupenda wewe daima....ili mwisho nije kwako juu mbinguni. Nimekosa Bwana, matatizo mengi.....wewe pekee unakuwa msaidizi wangu, unanipa mbinu ya kutatua ninabaki na furaha daima!
Nilipokuwa na madhambi mengi, wewe ukaja ulimwenguni....ukakaa pale juu ya msalaba ili kuyafuta madhambi yangu. Hata nikikosa wewe Bwana upo tu huniachi, nikitubu unanisamehe....na upendo huu unanifundisha kusamehe wanao nikosea!
No comments:
Post a Comment