Wednesday, December 7, 2011
ANGALIA SASA HAWA JAMAA....NDO KABISAAA!!!!!!
Hawa jamaa wa mabasi....ndo wendawazimu kabisa, utafikiri huwa wanabeba magunia kumbe binadamu kabisa....hivi kweli ikitokea ajali hapa utasema bahati mbaya kweli? Eti watu husema kazi ya Mungu, mbona tunamsingizia sana Mwenyezi Mungu....kwa upumbavu wetu, Mungu katupa akili tuzitumie vizuri, sasa hawa utawaita wenye akili timamu kweli? Kona, mlima...ambapo huoni mbele kabisa, tena watatu wanafuatana. Kwakweli bado tuna kazi sana! Mpaka kujikomboa na mawazo ya utumwa wa akili itachukua muda sana....maana bado ni watumwa tu wa akili...kweli ukiwa huru mwenye akili timamu utafanya kitu kama hiki?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment