Hatari lakini salama.....gari la Mkuu Mwenyekiti Mjengwa lapata ajali, lakini hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kuumia, Mwenyezi Mungu ashukuriwe. Mkuu Mjengwa namfahamu kwa ukaribu sana, na nimekutana naye mara 3 hivi na gari lake hili, ninalifahamu nikiliona tu! najua Mkuu Mjengwa yupo mitaa hii...gari hili limekuwa kama kielelezo chake Mkuu Mjengwa. Mwezi wa 9 nilikutana naye Dodoma, kabla sijamwona niliona gari lake hili limepaki sehemu nikajua yupo mitaa ya Dom, hivyo sikusita kumtafuta na kuonana naye na kufurahi pamoja.
- Pole zangu kwa Mkuu Mwenyekiti wetu wa Blog ya Mjengwa, kwa kupata shida na gari lake....naamini litarekebishwa na kurudi barabarani. Kila lakheri Mkuu Mwenyekiti Mjengwa!
No comments:
Post a Comment