Tuesday, December 6, 2011

HIVI MADEREVA TANZANIA....WATAKUJA KUELIMIKA LINI JAMANI?

Ningependa sana kuona wahusika wakiona hii picha washughulike mara moja, ukiona tu kama hivi, unachukua namba la hili gari na kulitafuta....kisha kumshughulikia ipasavyo tena kumfungia kabisa kuto kuendesha, au ikiwezekana kumfunga kifungo cha muda mfupi, lakini kazi ngumu.....nafikiri madereva wangeanza kushika adabu zao. Kila kukicha tunaona ajali za kizembe zembe zinazoua watu wengi sana wasio na hatia yoyote....hivi kweli ina maana Polisi na vyombo vya usalama barabarani havioni mambo haya? Haya sasa hebu oneni hapa...na mshughulikieni huyu jamaa wa hii Benzi nyeusi, au mnamwogopa? Jamani chonde chonde okoeni maisha ya watu kwa kuwazibiti watu kama hawa wanaovunja sheria za barabarani. Mbona wenzetu wanaweza....kwanini sisi tusiweze kuzibiti mambo kama haya...ili kupunguza ajali zisizo za lazima, lini mtaanza kuwa makini kwenye kazi zenu, au mpaka Taifa liteketee lote kwa ajali za barabarani?

No comments:

WATEMBELEAJI