Monday, December 26, 2011

JUMATATU YA NOELI NI SIKU YA FAMILIA TAKATIFU!



FAMILIA TAKATIFU YA YESU, MARIA NA YOSEFU!


Wachungaji wakaenda kwa haraka wakamkuta Maria na Yosefu, na yule mtoto mchanga amelala horini.


Salamu Mama mtakatifu wa Mungu....uliyemzaa Mfalme mwenye kutawala mbingu na dunia daima na milele!


- Wito wangu ni tutunze na kujali sana Familia zetu, kwani ndio msingi bora wa maisha yetu; tuige mfano mzuri wa Mama Maria na Yosefu; walivyoishi huko Nazareth kwa amani na upendo. Walishirikiana siku zote, walipendana mapendo ya kweli na kuheshimu ndugu na jirani na kuwasaidia. Walivumilia shida mbalimbali na kuzikabili....hivyo hatuna budi kuiga Familia hii Takatifu, na kuiomba itusaidia katika kusonga mbela na Familia zetu. Mama Maria Mama yetu mwema sana....na wewe ndiwe tegemeo langu kubwa sana, nakuomba sana uzijalie Familia zote ziwe na amani na mapendo daima, pia kwa vijana wote wanaojiandaa kuwa na familia kama mimi, basi uweke mkono wako wenye neema nyingi na kutuombea zaidi na zaidi kwa Mungu baba, kupitia kwa Mwanao Mpendwa Yesu Kristu, ili tufanikiwe kuchagua vyema wachumba wema na hatimaye tungane kuwa mwili mmoja katika Kristu. Tunakuomba sana mama Maria ututazame kwa huruma na kutusimamia ipasavyo!

No comments:

WATEMBELEAJI