Thursday, December 29, 2011

KATI YA WABUNGE NINAO WAKUBALI NI HUYU JANUARI MAKAMBA!

Agosti 2011...katika viwanja vya Bunge, Mjini Dodoma. Pamoja na Mbunge kijana kabisa Januari Makamba, wa kwanza kushoto.




Karibu sasa mwaka unaisha huu wa 2011, nilikuwa natafakari sana kuhusu viongozi wetu wa Serikali yetu ya Tanzania. Imetokea kumpenda Mbunge huyu kijana kabisa wa Bumbuli si mwingine ni; Januari Makamba.....nilipata bahati ya kuhudhuria vikao vya Bunge mara 4 mwaka huu, nilikuwa nasikiliza kwa makini sana jinsi waheshimiwa wanavyo ongea Bungeni hapo. Mazungumzo na sera za Mh.Januari Makamba, nilizipenda sana pamoja na zile za Mh.Mama Anna Kilango Malecela...nasema hivi kwa moyo wangu wote bila kuwa mpambe au mnafiki, maana watu tunapenda sana kusifia tu bila kuwa waangalifu au wakati mwingine kutaka kujipendekeza kwa watu kama hawa mhimu. Nilipendezwa na hawa waheshimia kwasababu wanasema mambo ya kweli, ambayo yalinigusa sana....na kama wanasema kweli yanatoka moyoni mwao basi wanastahili kuwa katika nyazifa za juu sana, ili waweze kutetea kweli wanyonge Watanzania ambao wanahangaika sana katika matatizo na maisha magumu sana. Hasa kama Mbunge huyu Mh.January Makamba, ambaye ni kijana kabisa na ndiyo mara yake ya kwanza kuingia Bungeni, basi endeleza zaidi na zaidi libeneke Mheshimiwa, sitaki kuwasifia sana ila nataka kusema;


- Nawatakieni kila lakheri kwa moyo wangu wote, ili kweli Mwenyezi Mungu awatie nguvu ya kutokata tamaa ya kutetea wanyonge na kupambana ipasavyo bila kuogopa mtu yoyote katika kutetea Wanyonge wa Tanzania, ambao wanahitaji sana msaada ya kutetewa ipasavyo. Ujumbe huu sijui kama utawafikia wenyewe....lakini sijali, ila naamini kabisa tena kwa dhati kabisa sala zangu kwao zimemfikia Mwenyezi Mungu.

Nilipata bahati ya kukutana na Waheshimiwa hawa kwa muda mfupi na kupiga nao picha na kuongea walau kidogo, nilipata picha nzuri sana...kuwa ni watu wa kweli, kwa watu wote...bila kuwa na malingo na majivuno kama viongizi wengine, mapozi kwa sana...utafikiri wao sijui akina nani, dunia hii tunapita tu; hata uwe nani utapita tu!


Ujumbe wangu na ushauri; Mh.Januari tetea watu wako bila kuogopa kitu, Mama Kilango sauti yako Bungeni iwe kali sana zaidi na zaidi, na machozi yako yamwagike kweli kama nilivyo kuona katika kutetea Wanyonge ambao wanataabika sana. Naamini Mwenyezi Mungu atawalipa kwa yote mfanyayo!


- Big Up...sana Mh.Januari na Mama Kilango.




No comments:

WATEMBELEAJI