Dada mwenye mtoto mchanga aliingia ndani ya Basi kupitia mlango uliyo karibu na dereva...dereva alipomwona mtoto wa huyo msichana akamwambia; '' Hakya nani tena dada sikuwahi kuona mtoto mwenye sura mbaya kama huyo wa kwako....sipati picha Baba yake atakuwaje''
Mdada akiwa amekasirika sana akaenda nyuma kabisa ya basi kukaa, akakaa na Baba mmoja mtu mzima wa makamo. Dada akamwambia yule Baba; dereva wa basi hili amenidhalilisha sana leo kwakweli.
Huyo Baba wa karibu yake akamwambia; usikubali hata kidogo, nenda mbele kamwambie ukweli, na wakati unaenda unaweza kuniachia huyo Nyani wako nikuangalizie.
Dada wa watu akazimia.
No comments:
Post a Comment