Friday, December 23, 2011

LORI 3 ZA JESHI LA ITALY...KWAAJILI YA MLADI WA MAJI DODOMA!

Leo nimesafiri mpaka hapa sehemu ya Mji wa Modena-Italy, kukagua Lori tatu ambazo zitaenda huko Dodoma - Tanzania, kwaajili ya Water Project....mradi wa Maji Vijijini. Ni Lori ambazo zinafaa sana kwa mambo ya Vijijini, ni ngumu sana zinapita kila sehemu...ambapo ni shida kwa Lori nyingine kupita, nakumbuka nikiwa Dodoma tulisafiri na hizi Lori maporini, ilikuwa ni kama mchezo, zinapita kwenye mabonde, kwenye Mito yenye maji ya kuogopa...lakini tulipasua tu. Hivyo hizi Lori 3 zitakuwa msaada mkubwa sana katika Project hiyo ya Maji Vijijini. Wataanza kurekebisha, marekebisho kidogo na kupaka rangi, ili kuwa rangi ya kawaida sio ya Kijeshi, na baada ya hapo tutazisafirisha kwenda Dodoma - Tanzania.




Dodoma Lori hizi tulikuwa tukiziita; Banyamulenge au ukipenda Nyumbu.

No comments:

WATEMBELEAJI