Sunday, December 25, 2011

MANENO MAZURI YA SIKUKUU YA CHRSTMAS!

Mtoto amezaliwa na Mwana ametolewa kwetu, katika mabega yake hukaa Utawala wa Dunia. Habari njema ya Noeli ni kuja kwake Mungu kwa wanadamu...Mungu hakai nasi mbali, bali amejiunga nasi...anakaa nasi daima!

Bwana aliniambia; ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa....tufurahi sote katika Bwana, kwasababu Mwokozi wetu amezaliwa duniani. Leo amani ya kweli imetushukia toka mbinguni. Neno limefanyika mwili, nasi tumeuona utukufu wake.
Kwaajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume na uweza wa kifalme utakuwa mabegani mwake....naye ataitwa jina lake; mshauri wa ajabu!


- Na mimi leo nimefurahi sana, maana wajina wangu amezaliwa; maana mimi jina langu la ubatizo ni; Emanuel....basi tu limezoeleka jina la Baraka mpaka la Emanuel limefifia kabisa.

No comments:

WATEMBELEAJI