Msanii na aliyekuwa Mmiliki wa Motika Records na Mwanamziki wa kizazi kipya....wa kwanza aliyekuwa akiimba nyimbo zake kwa miondoko ya Kabila lake la Kimasai, Abel Motika a.k.a Mr.Ebbo (Pichani) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, baada ya kuugua kwa muda kidogo tu huko Mkoani Tanga, alikokua anaishi. Mipango ya kusafirisha mwili wa Marehemu kuelekea Jijini Arusha nyumbani kwao kwa mazishi unafanywa.
Mr.Ebbo katika uhai wake alitamba sana na nyimbo kama Mimi Mmasai Bwana, Kamongo na Boda boda na nyingine nyingi tu.
- Mimi binafsi nilikuwa nampenda sana Msanii huyu Mr.Ebbo, nimesikitishwa sana kupokea taarifa hii ya kifo chake, nilikuwa napenda sana nyimbo zake alikuwa anachekesha sana; hasa wimbo wa albamu yake ya mwisho iitwayo ALIBAMU wimbo ule wa; Acha hiyo tabia mbaya...kwakweli alichekesha sana na kusema ukweli jinsi tunavyoishi Tanzania na Tabia zetu mbaya.
Blog hii ya KAZI YAKO NI JINA LAKO; Kwa masikitiko makubwa sana inaungana na Waombolezaji wote katika kipindi hiki kigumu cha msiba huu mzito wa ndugu yetu Mr.Ebbo. Na kumwombea sana Mwenyezi Mungu aiweke Roho ya Marehemu mahali pema peponi.....Amina!
1 comment:
Marehemu na astarehe mahali pema popeni. Amina.
Post a Comment