Sunday, December 18, 2011

MSIBA WA MAMA HUYU...AMBAYE NILIMFAHAMU KWA UKARIBU SANA!

Mama huyu, Mama Pia.....ambaye nimekuwa naye karibu sana katika ushauri, kujifunza mambo mbalimbali ya mila na desturi za hapa Italy, na tena ndiye yeye aliyenifundisha Lugha ya Kiitaliano na kiluga cha hapa kiRomagnolo, yeye alikuwa Mwalimu wa shule ya Msingi miaka ya nyuma. Siku za mwanzoni kabisa wakati nafika tu hapa Italy, yeye ndiye aliyenipokea kwa ukaribu sana....na kuwa Mama yangu Mlezi kabisa, kwa upendo aliokuwa nao kwangu. Leo hii nimepata taarifa amefariki ghafla tu, mchana alikuwa anakula na alianza kujisikia vibaya basi ndo mauti yakamkuta, siku tatu zilizopita nilikuwa kwake nyumbani, alikuwa mzima wa afya njema kabisa....pia Ijumaa jioni niliongea naye kwenye simu vizuri tu, leo naambiwa hayupo nasi tena...kwakweli machozi yamenitoka nilishindwa kujizuia; maana alikuwa kama Mama yangu kabisa....hata nikiwa nyumbani Tanzania likizo alikuwa ananipigia simu mara kwa mara na kunijulia hali. Leo mchana nilipata tarifa hii ya huzuni sana ya kifo chake cha ghafla, nilikimbia haraka hapo nyumbani kwake, lakini sikufanikiwa kuwahi kwani walishampeleka Mochwari - Hospitali, nikaenda Hospitali haraka ili kumwaga kwa mara ya mwisho lakini sikufanikiwa, walisema mpaka kesho mchana ndipo tutaruhusiwa kuaga, maana huku ukichelewa unaweza usiage kabisa, wanafunga sanduku mapema. Kwakweli sisi binadamu ni wapitaji njia tu....hatujui siku wala saa, hivyo hatuna budi kuwa tayari wakati wowote na kuwa watu wema, ona sasa hapa alikuwa anakula tu! mauti yakamkuta. Wakati huo wa nyuma Kabla sijamaliza mwaka hapa Italy nilikata tamaa kabisa, nilitaka kurudi Tanzania tena nilikuwa nimeshafungasha kabisa kurudi, lakini mama huyu alinisii sana na kunifariji mpaka nikaamua kubaki, na baada ya kuisha mwaka alinifanyia sikukuu ya kunipongeza kukubali kubaki Italy, nitamkumbuka daima kwa pendo wake Mama Pia. Amefariki akiwa na miaka 75, lakini ungemwona alikuwa bado mwenye nguvu sana na mwenye afya njema kabisa. Kwangu mimi tena hili ni pigo jingine......lakini yote ni ya kumshukuru Mwenyezi Mungu.
-Mungu ailaze mahali pema peponi roho yako Mama Pia....Amina!

Pamoja na Pia. Nyumbani kwa Mama Pia.....nilikuwa nimepazoea kama nyumbani kwangu kabisa, wakati wowote nilikuwa naenda kama mtoto wa nyumbani kabisa. Nilikuwa nikisema leo nakuja kula kwako Mama Pia; ananijibu; haina haja hata ya kuniomba. Mama huyu alikuwa na upendo wake wa pekee kabisa. Alikuwa ananiambia daima; Mimi sijapata bahati ya kuwa na watoto, wewe kama mtoto wangu kabisa.



Mimi na Mama Pia...siku ya kwanza kwanza kunitembeza kwenye Barafu, nikiwa mgeni kutoka Tanzania.





Birthday yangu ya kwanza kuifanya nchini Italy....niliandaliwa kwa shangwe sana na Mama huyu Pia, ambaye sasa ni marehemu sasa.

















Niliandaliwa nyumbani kwa Mama Pia...sikukuu yangu ya kutimiza mwaka mmoja wa kuishi Italy.


- Nitakukumbuka daima Mama Pia.....Mwenyezi Mungu akupokee kwa amani kwenye makao yake ya milele huko Mbinguni. Amina.










1 comment:

Anonymous said...

pole sana kaka najua kwa jinsi gani umeumia haswa ukizingatia ya kwamba huyo mama alikuwa ni zaidi ya rafiki kwako wewe ulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi hiyo ni njia ya sisi sote ni kwamba tu huyo ametutangulia nasisi tutafuata ni kwamba tu kifo hikizooleki maana ingekuwa tungesha zoea iliyobaki ni tuwaombee waliotutangulia Amini

WATEMBELEAJI