Salamu sana Wadau wangu wote....Salamu sana pia katika siku hii ya leo Jubilee ya 50 ya Uhuru wetu. Nawatakieni sikukuu njema sana na yenye furaha tele na amani kwa wingi....kama ilivyo kawaida ya nchi yetu ya Tanzania. Pia nawashukuru wote kwa moyo wangu wote kwa kunipa pole na kunifariji kwa kufiwa na Mpendwa Babu yangu. Nawashukuruni sana tena sana kwa moyo wenu wa upendo kwa kuwa nami karibu katika swala hili la msiba...asanteni sana! Basi maisha nayo yanaendelea kama kawaida; Nipo safarini kuelekea huko Mjini Roma kuungana na wenzangu/Watanzania wenzangu katika kusherekea sikukuu hii ya miaka 50 ya Uhuru wetu. Sherehe itaanza jioni nami naamini nitakuwa tayari nimeshafika huko kwa neema za Mwenyezi Mungu, ili kuitikia mwaliko wa Watanzania wenzangu...walionialika kwa upendo, na kusema; usikose tafadhari....nami nimeitikia wito huu kwa moyo wote. Asanteni sana Wana Jumuiya ya Roma kwa mwaliko.
Tanzania oyeeeeeee....!!!!!! Uhuru wa 50 oyeeeeeeeee!!!!!!!!
No comments:
Post a Comment