Thursday, December 29, 2011

RC..DODOMA ATAKA THAMANI STAHIKI YA MIRADI.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.Rehema Nchimbi...amewataka watendaji Serikalini kuwa waaminifu ili miradi inayotekelezwa iwe na thamani inayostahili....Dk.Nchimbi, alisema hayo wakati akizindua Mradi wa Maji wa Hombolo Makulu, uliofadhiliwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Dodoma kwa ushirikiano na Shirika la Wakapuchini la Uholanzi. Dk.Nchimbi, alisema; kuna haja kwa viongozi wa Serikalini kujifunza, mapato na matumizi ili kila mradi unaotekelezwa uwe na thamani inayolingana na fedha zilizotolewa.
''Kwanini sisi tusiige mfano huu katika uaminifu tunapotumikia Serikali au katika vyama vyetu vya siasa....fikra na maadili vibadilike tukiwa na hofu ya Mwenyezi Mungu. Mradi huu umegharimu Shilingi Milioni 34, lakini ungekuwa wa Serikali tungeambiwa umegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 100'' alisema hivi Dk.Nchimbi.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki (Caritas) ambaye pia ni msimamizi wa Miradi ya Kanisa katoliki Jimbo la Dodoma, Padri Sergio Madinda...alisema; Mradi wa maji Hombolo Makulu ulianza Novemba 12, Mwaka huu na kukamilika Desemba 28, Mwaka huu. Umegharimu Shilingi Milioni 34, Mradi huu ni wa Wana Hombolo Makulu, hivyo matarajio yetu kuwa watautunza, wataweka utaratibu mzuri wa kuchangia huduma ya maji ili kudumisha uendeshaji wake na sisi tupo tayari kushirikiana nao kikamilifu katika swala hili zima...alisema haya Padri Sergio Madinda.

- Habari na Sifa Lubasi - Dodoma.

No comments:

WATEMBELEAJI