Friday, December 9, 2011

SALA YA KUIOMBEA TANZANIA!


Ee Mwenyezi Mungu, asili ya kila kilicho chema, tunakushukuru kwa mema yote uliyotujalia sisi Watanzania....tunapoazimisha Jubilee ya miaka hamsini ya Uhuru tunakushukuru kwa kutuwezesha kuishi maisha mema kama iwastahilivyo wana wa Mungu. Kwa kutumia busara za Waasisi wa Taifa letu umetujalia tuwe Taifa moja lililounganika katika umoja, upendo, amani na mshikamano wa Kitaifa.
Tunaweka mbele yako Baba changamoto nzito linalo likabili Taifa hili na mambo yote yaliyo kinyume kabisa na mpango wako wa kutaka tuishi kwa amani, zishindwe kuathiri tunu bora ulizotujalia.

Tunawaombea Waasisi wa Uhuru huu wa nchi hii, kwa namna ya pekee Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na mwenzie Amani Abed karume, waliotutangulia uwapumzishe kwa amani kwako mbinguni. Nasi utufadhilie kufikia ukomo uliyotutayarishia wewe Baba Mungu, wa kuwa raia katika ufalme wako wa mbinguni milele yote.

- Mungu Ibariki Tanzania na watu wake wote....amina!

No comments:

WATEMBELEAJI