Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa mema yote aliyonijalia katika Mwaka huu wa 2011. Sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote kabisa, bila yeye mimi nisingelikuwa hapa leo!
Pili napenda kuwashukuruni ninyi nyote Wadau wangu wa kijiwe hiki cha; KAZI YAKO NI JINA LAKO, bila nyinyi kijiwe hiki si kitu kabisa hivyo ninawashukuru sana tena sana kwa kutembelea kwenu hapa. Pia nawatakieni mafanikio mema mengi sana katika mwaka ujao wa 2012 uwe Mwaka wa neema sana na wa mafanikio tele kwenu ninyi nyote Wadau wangu.
- Basi leo ni mwisho wa Mwaka 2011, hivyo hatuna budi kushukuru kwa yote aliyotujalia Mwaka huu wa 2011. Tunapojiandaa kuupokea Mwaka mpya wa 2012 usiku huu, tutasherekea kwa shangwe sana....ila tusisahau kusherekea vizuri bila fujo na kusahau wenzetu walio na shida mbalimbali.
Basi niwatakieni mwisho wa Mwaka wenye heri na fanaka nyingi sana.
- Kila lakheri kwa yote......Pamoja daima!
Chibiriti.
No comments:
Post a Comment