Sunday, December 11, 2011

TAFAKARI YANGU KATIKA JUMAPILI HII YA LEO!

Chini ya jua kila kitu umekiumba wewe, Mungu wewe wastahili sifa zote....uhimidiwe milele yote. Tazama ndege wa angani asubuhi na mapema wanakusifu kwa sauti nzuri....wakisifu uumbaji wako mzuri, kwanini mimi mwanadamu nisikutukuze Mungu wangu.
Nikuimbie wimbo gani? wenye tenzi nzuri za kutukuza ukuu wako....kutakasa uumbaji wako Mungu mkuu. Ee Bwana wewe ndiwe mkuu, usifananishwe na kitu chochote kilichomo duniani, kwa matendo yako makuu tena ya ajabu sana.
Mwanadamu ni kitu gani? hata umkumbuke? tena atenda maovu mengi....nawe Mwenyezi Mungu unasamehe, hakika huruma yako Mungu ni ya pekee sana.

No comments:

WATEMBELEAJI