Thursday, December 15, 2011

VIFO VYA HAWA WAAFRIKA WENZETU....VIMENIUMA SANA!

Nchini hapa Italy....juzi limetokea jambo baya sana kwa Waafrika wezetu kutoka huko nchini Senegal. Wameuwawa kikatili sana na Jamaa mmoja Mwitaly...ambaye alikuwa akichukia sana watu Weusi (Mbaguzi wa rangi)...alituchukia mpaka kufikia uamzi wa kuwashuti kwa bunduki hawa vijana wasio na hatia yoyote ambao walikuja Italy kujitafutia mahitaji yako kutokana na hali ngumu ya maisha nchini kwao. Jamaa aliwapiga risasi na baadaye kujiua na yeye kwa kujishuti, pia kujeruhi wengine wengi ambao kwasasa wapo Hospitalini na hali zao ni mbaya sana. Yaani nimeshitushwa sana na hili jambo mbaya sana.....na sikutegemea kabisa nchi kama hii ya Italia bado kuna ubaguzi wa rangi na chuki za Watu weusi kama hivi? Vijana wa watu walikuwa hawana kosa lolote wakitembea tu barabarani....bila wasiwasi wowote, na mara mauti yakawakuta kwa hasira zisizo na msingi wowote...tena alikuwa hawafahamu hata kidogo, kwasababu ni weusi tu basi ikawa ni shida kwake. Tena kingine nimesikitishwa sana na Habari hii ambapo vymbo vya habari na TV hawakutilia mkazo wa jambo lilivyobaya....wanaliongelea ki uraisi raisi tu, je mtu Mweusi angefanya hivi ingekuwaje? Kwasasa ingekuwa skendo kubwa na kuongelewa kila mara, na kusaka Watu weusi wote na kuwarudisha makwao hata kama hawana hatia yoyote. Kweli ubaguzi wa rangi bado upo sana tena sana tu hapa duniani, na sikutegemea kabisa nchi kama Italy iwe hivi. Nimekasirishwa sana na kusikitika sana katika jambo hili.

- Mungu azilaze pema peponi roho za Marehemu hawa wasio na hatia yoyote....amina!

No comments:

WATEMBELEAJI