Huwa nawaza sana na kujiuliza sana....hivi lini umeme utakuja kuwaka moja kwa moja bila kuzima Tanzania yetu? Maana mmmhhh.....nipo huku Ugaibuni huu Mwaka wa 11 sasa sijawahi kuona hata siku moja umeme ukatike, yaani sikumbuki kabisa lini ulikatika....labda itokee itirafu kweli, napo ni kwa muda mchache sana wanakuwa tayari wamerekebisha shida. Sasa na kwetu lini? Hasa kwa Dar es salaam a.k.a Bongo huwa ni kero sana, Dodoma huwa ni afadhali sana hasa likiwepo Bunge basi sisi wa Dodoma husahau kabisa kama kuna mgao wa umeme, wakiondoka tu waheshimiwa....basi utaona hata umeme unaanza kusuasua, lakini siyo ki hivyo kama Dar es salaam.Siku nilipokutana na huyu Jamaa pichani Mh.Ngeleja, Waziri wa Nishati na Madini... pale Dodoma, hapo hapo swali langu lilikuwa hili; Mheshimiwa lini tutafanikiwa kupata umeme wa moja kwa moja? Jamaa alinijibu; endelea kuota tu....ndoto yako ipo siku itakuja kutimia, akanianzishia utani wewe si Chibiriti, washa unasubiri nini? Basi kwasababu ni mtani wangu...ikabidi ninywee tu! Ila jamaa anachekesha kweli, tulicheka na kufurahi yakaisha. Ila huwa nasikitika sana kuhusu maswala muhimu kama ya maji na umeme, yanakuwa hayapewi nafasi ya juu na kutiliwa mkazo jinsi ipasavyo....mpaka aibu. Kwa wageni huwa kwao ni ajabu sana, na wanashangaa sana na kutoamini. Sasa je lini utawaka moja kwa moja, bila watu kuusubiria kwa masikitiko na ukirudi watu; Huooooooo!!!!! ?????
No comments:
Post a Comment