Monday, January 30, 2012

JAMANI HAYA MAMBO SASA NI MAZITO........!!!!!!!

Pichani ni; Mwanahija Cheka, a.k.a ''Bibi Cheka'' ambaye kwasasa ana umri wa miaka 51 ambaye hajulikani sana katika medani ya Muziki, ameamua kujitosa kuimba Muziki wa Kizazi kipya na kurekodi wimbo uitwao; NI WEWE.
Meneja wa TMK Wanaume Family, Ndg.Saidi Fella, a.k.a ''Mkubwa Fella'' aliweka wazi kuwa katika wimbo huo umerekodiwa Studio ya Poteza Records, amemshirikisha kinara wa Kundi la TMK, Amani Temba, a.k.a Mh.Temba. Mkubwa Fella...alisema kuwa; licha ya kutojulikana sana kwenye medani ya Muziki, lakini uwezo wa Bibi Cheka katika kuimba na kurap ni mkubwa sana.
Huyu Mama watu wengi hawamjui lakini mimi nasema; huyu ni Mwanamuziki kabisa....alikosa nafasi tu ya kudhihirisha uwezo wake....alisema hivi; ''Mkubwa Fella''.

- Picha na Habari na Mkuu Lukwangule.

No comments:

WATEMBELEAJI