Sunday, January 15, 2012

LEO NI LEO NDANI YA UWANJA WA SAN SIRO a.k.a MEAZZA.

Leo ni leo ndani ya Uwanja wa Meazza - San Siro, huko mjini Milan - Italy. Ambapo watani wa Jadi kati ya Ac.Milan na InterMilan, wakishuka uwanjani baada ya dakika kadhaa zijazo kupambana mpambano mkali wa upinzani, ni maarufu sana hapa Italy...wanaita; Derby della Madonnina....sasa nani atatoka mshindi? Tusubiri hapo baadae. Mimi ni mpenzi na Mshabiki sana wa Ac.Milan, sikupata tu Ticket ya kwenda kuangalia huko Milano, la sivyo leo ningekuwa huko, nilikosa kutokana na kujua ningekuwa huko Ujerumani, lakini ratiba ikabadilika nikajikuta nimerudi hapa Italy, bahati mbaya nimekosa Ticket, ila nipo njiani kwenda kwenye Baa yangu maarufu ya washabiki wenzangu na wale Wapinzani wetu wa Inter, huwa tunachanganyikana pamoja, basi ni matusi kwenda mbele na raha mtindo mmoja...baada ya Mechi kuisha huwa ni vilio tu, kwa kushindwa...sasa leo ni nani zaidi Ac.Milan au InterMilan? FORZA MILAN.



No comments:

WATEMBELEAJI