Matembezi ya kupanda mlima kwaajili ya kusaidia Watoto Yatima wa Makalala - Mafinga - Iringa. Mnamo Mwaka 2006 marafiki hawa waliamua kunialika kufanya matembezi ya porini na kupanda Mlima mkali, wao waliamua hivyo na kusema matembezi haya yatalenga zaidi na kuchangia Watoto Yatima, walinialika nami nikajiunga nao na kuchangia mchango maalumu kuwachangia Watoto hao. Nilifurahishwa sana na jambo hili zuri.....la kukaa pamoja kwa siku 2 huko porini na kufanya matembezi, ila matembezi yenyewe yalikuwa magumu sana maana ilikuwa ni kupanda milima usiambiwe, lakini nilifurahi sana. Na leo tena nimepata taarifa kuwa wanaandaa matembezi mengine ili kukaa na kufurahi pamoja na kukumbuka wenzetu wasio na uwezekano wa kuishi vizuri, yaani umaskini wa kupungukiwa maisha kamili kama ipasavyo kuishi kwa kila mwanadamu. Mimi jibu langu lilikuwa ni; lazima niwepo tena hata kama kesho nipo tayari kwa matembezi hayo.
Hapa ni sehemu tulipo lala kwa siku 2, ni katikati ya pori na kuzungukwa na milima mikubwa miwili. Hapa tulikuwa katika maandalizi ya kuanza kutembea kwa kupanda Mlima, na ndio ilikuwa siku ya kwanza ya matembezi haya.
Katika kukatisha kijimto kidogo......
Hapa Mlima au mwinuko unaanza sasa.....hapa ugumu kwenda mbele unaanza sasa.
Taratibu lakini....tuliweza kufika kileleni.
Sara, Serena na Rosella..... hapa matembezi yamekubali. Jumla tulikuwa 7, wanawake 5 na sisi wanaume 2.
Mapumziko kidogo.......baada ya ugumu wa kupanda Mlima.
Picha zingine zitaendelea hapo kesho.........
No comments:
Post a Comment