Wednesday, January 18, 2012

SAFARI YA MWISHO YA MH.REGIA MTEMA...MJINI IFAKARA -MORO!.

Kwaheri Mheshimiwa Regia, safiri salama na upumzike kwa amani....tutakumiss sana tu! Lakini basi ni mapenzi yake Mwenyezi Mungu. Ulale mahali pema peponi...amina!

Baadhi ya Waombolezaji wakiwa kwenye Mazishi ya Marehemu Regia Mtema...huko Ifakara.
Kwaya ya Ifakara....ikiimba Mapambio, katika Mazishi ya Mheshimiwa Regia.
Vilio na majonzi.....
Pacha wa Marehemu (Remija) akibembelezwa.
Mdogo wa Marehemu kwa huzuni, akiwa na msalaba wa Marehemu Dada yake Regia...msalaba ni ishara ya ukombozi na ufufuko.
Rais JK, akiongea jambo na Spika wa Bunge la Tanzania, Mh.Anne Makinda...msibani hapo!

Baadhi ya Wabunge toka vyama mbalimbali wakiwa mazishini.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu likishushwa kutoka kwenye Ambulance...tayari kupelekwa makaburini kwa mazishi.
Mwili wa Marehemu Regia ukiwasili Makaburini, tayari kwa kuzikwa.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh.Freeman Mbowe...akiwasili Makaburini.
Vijana wa Ulinzi wa CHADEMA Mazishini.....wakiweka watu sawa katika Ulinzi.
Umati wa Waombolezaji wakiwa Makaburini, katika Mazishi ya Mheshimiwa Mbunge wao.
Ibada ya Mazishi ikifanyika mbele ya Kaburi la Regia Mtema, kwenye nyumba yake ya milele...kabla ya kuzikwa.
Mh.Freeman Mbowe, akiweka udongo kaburini kwa Mh.Marehemu Regia.
Spika wa Bunge la Tanzania, Mh.Anne Makinda...akiweka udongo Kaburini kwa Mh.Marehemu Regia.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mh.Dkt.Wilbroad Slaa....akijiandaa kuweka Shada la Maua, kwenye nyumba ya milele ya Mh.Marehemu Regia Mtema.


- Picha kutoka kwa Mkuu Michuzi.

No comments:

WATEMBELEAJI