Saturday, January 14, 2012

MBUNGE WA VITI MAALUMU WA CHADEMA..AFARIKI DUNIA LEO!

Habari mbaya zilizoifikia Blog hii ni kwamba; Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema...Mh.Regia Mtama, amefariki dunia leo hii, katika ajali ya Gari iliyotokea maeneo ya Ruvu. Alikuwa akiendesha gari lake kuelekea huko Morogoro. Hapa Ruvu kuna nini jamani? maana ajali hazikosekani kila mara, muda mfupi uliopita Wamissionari Wakapuchini walipoteza maisha yao kwa ajali ya gari maeneo hayo hayo ya Ruvu. Mbunge Marehemu Regia Mtamwa, kutoka Kilombero (Chadema) Enzi za uhai wake katika viwanja vya Bunge Dodoma - Tanzania.

Marehemu Mbunge Mh.Regia Mtama, akiwa kwenye moja ya mikutano yake enzi za uhai wake.



- Blog hii kwa masikitiko makubwa inatoa pole kwa msiba huu mzito kwa wana ndugu wote na Wana Chadema wote kwa kuondokewa na mpendwa huyu. Mungu ametoa na Mungu ametwaa...jina lake libarikiwe! Poleni sana wote.

Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi Regia Mtama....Amina!



No comments:

WATEMBELEAJI