Meri ya shirika la Kiitaly ya Costa Concordia...yazama na kuua watu 3 na wengi kujeruhiwa, watu 70 bado hawajapatikana. Meri hii siku ilipofanyiwa uzinduzi rasmi miaka ya nyuma kidogo...kwa kawaida hutupa chupa ya kinywaji cha shampeni kutoka juu ya Meri ili ufunguzi uende vizuri, lakini siku hiyo chupa hiyo haikuvunjika...wanasema wenyewe huwa sio alama nzuri hiyo, sasa watu wengi hapa Italy wanaamini ni kweli kabisa kuhusu hilo la chupa kutovunjika, maana Meri hii imepata ajali ndogo 2 na sasa hii ndo ya 3 nafikiri na ya mwisho. Ni Meri kubwa sana ya abiria...wanasema inakaribia ile ya Titanic. Chanzo cha ajali ni kugonga Mwamba, na bado uchunguzi unaendelea kujua zaidi kama ni makosa ya waendesha Meri hii au wale waelekezaji.







No comments:
Post a Comment