Monday, January 9, 2012

NIMEKUTANA NA HII KWENYE MTANDAO...NIMECHEKA NA KUUDHIKA PIA!

JAMANI SASA BINADAMU TUNAKWENDA WAPI? HUU SIO UUNGWANA HATA KIDOGO!!!!



Leo nilikuwa mitaa ya Temeke Jijini Dar es salaam, tulikwenda kwenye arobaini ya Jamaa yangu....nilichokiona hadi sasa sijaamini, kama kweli binadamu tumefikia hatua hii...kama mjuavyo siku ya hitima wafiwa wanaandaa misa na chakula, sasa nimefika pale mapema na watu walikuwa wengi, cha ajabu ilipokaribia mida ya chakula watu wengi vijana na wazee wakawa wanatoka, na kila anayerudi anakuja na kimfuko chake mkononi (ameshika hivi vimfuko laini) sikufuatilia sana...balaa ni pale tulipoanza kugawa chakula; heeee!!!! kila mtu anafungua kimfuko chake na kutoa ndizi mbivu na pilipili...anaanza kula! Kumbe walitokanavyo nyumbani kabisa! Nilipowauliza hapo baadaye....eti walisema; mbona siku hizi ni vitu vya kawaida tu! hususani Dar es salaam.
Kwani wana uhakika lazima siku kama hiyo, wali utakuwepo na wali bila ndizi mbivu na pilipili ya kutafunia haushuki vizuri? au hauliki kabisa? kwakweli siku hizi ubinadamu hakuna kabisa!


- Nilikutana na story hii kwenye mtandao, Jamaa akihathia...ilibidi nicheke sana na kusikitika sana, watu wanaweza wakakupania ufe, ili wale wali....kuhusu story hii; kweli nimeamini ule usemi usemao; KUFA KUFAANA.

No comments:

WATEMBELEAJI