Wednesday, January 11, 2012
NIMEREJEA ITALY LEO JIONI KUTOKA HUKO UJERUMANI.
Nimerejea leo jioni hapa Italy nikitokea Ujerumani, ilikuwa nikae Mwezi mmoja huko Ujerumani, lakini basi imenibidi nirudi tu......kutokana na sababu za hapa na pale, nimesikitika kidogo maana nilianza kuzoea huko Ujerumani ingawa Kijerumani ni kigumu, lakini nilianza kufurahia sana kuishi huko Ujerumani. Basi ndo maisha yanavyokwenda huwezi kuwa na kila kitu katika maisha haya, lazima wakati mwingine ukubaliane na mabadiliko yanavyokuja. Sasa naanza kujiandaa na safari ya kwenda Bongo, ambayo itakuwa hivi karibuni ila bado sijui lini, nimeambiwa hivi karibuni...hiyo safari ya kwenda Bongo ina furaha sana kuliko safari zote zote duniani. Ikishindikana hiyo hapo kweli nitachukia ki ukweli kweli.
Picha ya angani, wakati nikirudi toka Ujerumani....jamaa hawa huenda angani kweli kweli hadi mawingu huonekana chini haswa.

Inaitwa Milima ya Apenini....kwa kuiangalia kwa juu ni mizuri sana! Basi jamaa akifika hapa anatangaza kabisa na kugeuza Ndege pande zote mbili, ili watu washangae.....na kuisifia kwa sana utafikiri Milima hii ipo pande za Italy tu!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment