Tuesday, January 3, 2012

NUSU YA WAPIGA KURA MAREKANI HAWAMTAKI OBAMA KULIKONI!

Uchaguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kuwa asilimia 50 ya wapiga kura nchini Marekani wanasema; Rais Obama hastahili kutawala kwa muhula wa pili. Uchaguzi huo uliofanywa na shirika la USA Today/Gallup kati ya Desemba 15-18. Pia unaonyesha kuwa asilimia 48 ya Wamarekani watawapigia kura Wagombea wa Chama cha Republican huku asilimia mbili wakisema hawana maoni. Umashuhuri wa Obama unaporomoka kwa kasi kutokana na sera zake potofu ambazo zimesababisha matatizo makubwa ya kiuchumi Marekani. Aidha Wamarekani wengi wanasema; Obama hajatekeleza kikamilifu ahadi zake za kupunguza idadi ya Wanajeshi wa Marekani katika maeneo mbalimbali ya dunia.

- Habari na Challii a.k.a ILYA.

No comments:

WATEMBELEAJI