Monday, January 16, 2012

PACHA WA MH.MBUNGE REGIA MTEMA...AKIELEZA KUHUSU KIFO!

Remija Mtema, Pacha wa marehemu Mbunge Regia Mtema....akiwa na gongo la marehemu pacha wake, alilokuwa akitembelea wakati wa uhai wake.
Remija Mtema (32) ameeleza alivyonusurika baada ya kushuka kwenye gari muda mfupi kabla ya ajali ya Pacha wake kutokea.
Remija ambaye ni kurwa wa marehemu Regia, alisema; Regia kabla ya ajali yake iliyosababisha kifo chake, alikuwa akitoa kauli za kutia moyo na za kutarajia kuonana tena. Tulitoka nyumbani kwake Mbezi - Makabe, Dar es salaam kwenye saa tatu asubuhi, mimi nilikuwa nakwenda Iringa na tuliondoka na gari lake hilo lililopata ajali....nyumbani hapo, wakanishusha Mbezi Stendi nikisubiri basi la Iringa. Wakati tunatoka nyumbani alikuwa akiongea kwa uchangamfu sana, kuanzia juzi Ijumaa tulizungumza na kupanga kwamba mimi niende Iringa kuomba ruhusa kazini, maana kuna wakati nikiwa huru namsaidia kazi kama Katibu wake. Tulipanga nikipewa ruhusa nirudi nimsaidie kwenye Kamati na Bungeni, ''alisema maneno haya pacha huyo Remija''

Kwa mujibu wa Remija, walikubaliana hivyo na baadaye kupanga mambo yao usiku huo wa Ijumaa, walicheza sana karata usiku huo huo......ni karata za kuagana maana mimi ndio nilikuwa nasafiri kesho yake kwenda Iringa, asubuhi ya Jumamosi ndipo tukaondoka huku tunacheka sana, mimi nikashuka Mbezi. Alikuwa zaidi ya Pacha wangu, alikuwa ni rafiki yangu sana, ''alisema Pacha huyu Remija''.
Remija ambaye ni Afisa Tarafa wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, anasema; aliposhuka Mbezi kusubiri Basi, alikaa naye pacha wake Regia na watu wengine kwenye gari kwa karibu saa moja, wakimsubiri Mama yao, Bernadeta....aliyekuwa akitokea Tabata - Chang'ombe nyumbani kwao. Mama alipofika aliingia garini na wakaondoka, Pacha Regia alisisitiza sana nikipata usafiri nimwambie, ni kama alitamani sana niende nao, lakini haikuwa hivyo. Baada ya muda wa nusu saa Mama alinipigia simu kuniuliza nimepata Basi, maana waliona Basi la Upendo limewapita.....nikamjibu; bado sijapata Basi, baada ya muda mfupi nikapata Basi la Budget. Nilipoingia kwenye Basi hilo saa tano asubuhi, nikamtumia ujumbe wa sms Regia kuwa nimepata Basi, lakini ujembe huo haukujibiwa....nikajua labda kwa kuwa alikuwa anaendesha gari, nikaendelea kusoma gazeti na tulipofika Ruvu niliona watu wengi sana lakini sikutilia maanani sana nikaendelea kusoma gazeti langu, ''alisema pacha huyu Remija''. Alisema; kabla hajafika Chalinze, alipigiwa simu na Mama yake kuwa wamepata ajali na wapo Hospitali ya Tumbi, hapo hapo nilimwomba dereva wa Basi anishushe kwakua ndugu zangu wamepata ajali Ruvu. Dereva na Kondakta wa Basi hilo waliniuliza aina gani ya gari? nikawaambia....wakathibitisha waliiona ajali hiyo, akasimamisha Basi hilo nikashuka na kuanza safari ya kurudi hadi Hospitali ya Tumbi, nikakuta Regia amefariki, ''alisema kwa uchungu sana Pacha huyu Remija''.

Alisema; Pacha wake alikuwa jasiri ambaye akiamua jambo ni lazima alifanye, alikuwa na huruma na asiyependa mtu yoyote aonewe, na alimwamini sana Mungu kwa kila jambo, kutokana na malezi ya Kiimani waliyopata kwa Baba na Mama yao.
Kwa mujibu wa Remija, yeye na Pacha wake Regia.....walizaliwa Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar es salaam, Aprili 21 Mwaka 1980.....Pacha wangu alikuwa Mpenzi na shabiki wa Timu ya mpira wa miguu ya Simba kwa hapa nchini na kwa nje alikuwa akipenda sana kufuatilia Barcelona ilipocheza, zaidi ya Timu nyingine.

Baba wa Marehemu, Estelatus Mtema - alisema; Namshukuru Mungu kwa kila jambo na kuomba majeruhi akiwemo mke wangu, waliolazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili....waliohamishiwa wakitokea Tumbi, wapone mapema.


- Habari na Gloria Tesha.

No comments:

WATEMBELEAJI