Monday, January 30, 2012

SHEREHE YA NDOA KAMA HII NAIPENDA SANA...HONGERA SANA!






Sherehe ya ndoa kama hii....mimi binafsi naipenda sana, maana haina gharama yoyote.....baada ya kufunga ndoa Kanisani maharusi na wasimamizi wao walijumuika kula pamoja.....sasa unataka nini hapa? Mimi napenda sana hivi, hata siku nikifunga ndoa yangu itakuwa hivi hivi labda hapa nitaongeza na wazazi na wadogo zangu basi. Mimi huwa sioni kabisa faida ya kufanya sherehe kubwa na kujitangaza kwa watu kuwa wewe ni wewe, wakati wengine wanahangaika sana hata kula kwa shida, wewe unachezea hela tu kwa kufanya sherehe za kifahari. Kwani ukifunga ndoa na kusherehekea kama hapa....ina maana utakuwa hujafunga ndoa au?
Wakati mwingine baada ya sherehe za kifahari kuisha, kinacho fuata ni tabu za kulipa madeni na karaha kibao, na nyinyi wenyewe wana ndoa ndani mnakuwa hamna kitu chochote...hata kuanza maisha inakuwa ngumu sana, sasa yote hayo ya nini? Cha muhimu upate baraka za Mwenyezi Mungu katika ndoa yako, hicho ndicho cha muhimu sana kuliko sherehe ya kifahari.
Tafakarini sana Wadau kuhusu swala hili..... na nawapa hongera sana hawa jamaa kwa kufanya sherehe kama hii....big up sana tu!

No comments:

WATEMBELEAJI