SIKUKUU YA BIKIRA MARIA MAMA WA MUNGU, JANUARI MOSI 2012.
Leo Mama Kanisa anasherehekea sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu, ''Theotokos'' ambayo huja daima kila tarehe Mosi ya mwezi januari. Ni sherehe ya amani kwa maana Mama Maria ni Mama wa amani. Amemzaa Mkombozi Mfalme wa amani na hivi Mama Kanisa anaona ni vema tukasali tukimwomba Mungu kwa njia ya Mama huyu kwa ajili ya amani ya ulimwengu.
Kauli mbiu inayoongoza maadhimisho ya siku ya kuombea amani duniani kwa Mwaka 2012 ''kuwaelimisha vijana katika haki na amani''..... Salamu Mama Mtakatifu wa Mungu uliyemzaa Mfalme mwenye kutawala mbingu na dunia daima na milele. Hii ndiyo salamu yetu kwa Mama mpendelevu Mama asiye na doa, ....katika sherehe hii tukufu tunapofungua Mwaka huu mpya wa 2012. Amani ni tunda ambalo latupasa kulipalilia daima katika maisha yetu!
No comments:
Post a Comment