Sunday, February 5, 2012

ENZI HIZO NIKIJARIBU JARIBU KIDOGO.

Nilikuwa napenda sana mambo haya, mpaka sasa bado napenda sana....ila muda sina, sikupata nafasi ya kujifunza vizuri....lakini napenda sana. Leo rafiki yangu mmoja wa huko Dodoma, ndg.Cosmas...amenipigia simu ya kunitakia heri ya kuzaliwa, basi tumeongea mengi sana na akanikumbusha wakati alikuwa akinifunza kupiga Kinanda, nimekumbuka mbali sana nikaamua niweke picha hii; hapa ilikuwa Mwaka 2005 nikiwa huko Imola kwa marafiki zangu kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Irene, ambaye yupo hapo kwenye picha nyuma....kalikuwa kasichana kadogo tu, sasa ni mama kabisa......tuliimba wimbo wa Happy Birthday-kwa Kiitaly kwaajili yake, nami nilipiga kinanda katika wimbo huo, akiwa na marafiki zake na wazazi wake (hawaonekani kwenye picha).

Cosmas, kwasasa mpiga Kinanda Kanisa Kuu la Dodoma, pale Jimboni.....amesema; amenizawadia kanda ya Kwaya ya Mt.Kizito Makuburi, nikienda nitaikuta......yeye anajua mimi ni mpenzi sana wa kwaya, na anajua kwaya zipi.....moja wapo ni hiyo ya Makuburi-Dar.
Huwa nanunua hata nisiposikiliza kabisa kwaya hizi nazipenda sana ni; Mt.Cesilia - Arusha na Mt.Kizito - Makuburi - Dar es salaam.

No comments:

WATEMBELEAJI