Ndinga za Kijeshi za Italy.....zikiwa kazini, kusaidia hali tete ya Barafu iliyoshuka kwa wingi kupita kiasi na kusababisha mambo mengi sana kusimama pia kuhatarisha maisha ya watu wengi....huduma hamna, simu, umeme, nk....., ukiangalia mpaka unaogopa barafu iliyopo, wasiwasi sasa upo kwenye mapaa....sijui kama yanaweza kuhimili mzigo mzito wa barafu, kwakweli hali ni mbaya sana hasa hapa nilipo Cesena sijui itakuwaje, nilienda asubuhi sokoni vitu ni vichache sana, tena vile muhimu havipatikani kabisa. Wanasema haijawahi kutokea hivi, ilishatokea miaka 30 iliyopita....lakini sio kwa wingi hivi.
Wasiwasi umehamia kwenye mapaa sasa....kwasasa ni barafu ya kawaida tu, kama unga vile....lakini ikianza kuganda ikawa Ice kabisa, je mapaa yatastahimili uzito?
Maswali yameanza sasa mtaani, na kuogopa vile vile kupo.....Ee Mwenyezi Mungu tusaidie!
No comments:
Post a Comment