Wednesday, March 28, 2012

BIASHARA HII NI YA MWALIMU AU MZAZI?


Mwanafunzi wa moja ya Shule za Msingi Iringa Mjini akiwa amebeba karai lililo na ndizi na bisi....akienda kuuza. Biashara hii haikufahamika mara moja ni ya nani kati ya Mzazi au Mwalimu, na je Watoto hawa watawezaje kweli kumsikiliza Mwalimu akifundisha au watakuwa wakiwaza usalama wa biashara na ni wakati gani utafika akaweze kuiuza. Ombi kwa Wazazi na Walimu wasiwape Watoto nafasi ya kufanya biashara hizi Shuleni, kwani; ni moja ya vitu ambavyo vinaathiri sana maendeleo yao ya Elimu darasani.

- Picha na Mkuu Mroki a.k.a Father Kidevu.

No comments:

WATEMBELEAJI