Friday, April 6, 2012

IJUMAA KUU: URITHI WA KIPEKEE KWA MAISHA YA MKRISTO!

WAUMINI WAKIWA KANISANI......KATIKA IJUMAA KUU.

Leo ni Ijumaa Kuu......Wakristu duniani kote wanajumuika siku ya leo kwenye nyumba za ibada mbalimbali kuadhimisha siku ya kifo cha Yesu Kristu, aliyeteswa na kusulubiwa msalabani na kukata roho ilipofika alasiri ya saa tisa.
Kwenye nyumba za ibada za Kikristo, ifikapo saa tisa alasiri ukimya hutawala, mishumaa huzimwa na kengele hupigwa, kuashiria majonzi ya mateso ya Yesu Kristu pale msalabani. Ijumaa kuu ni siku ambayo Wakristu duniani kote hukumbuka mateso aliyoyapata Yesu baada ya kusulubiwa msalabani, yapata zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita.

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeipa umuhimu na thamani kubwa siku hii, kwa kuitangaza kuwa ya mapumziko. Siku hii huadhimishwa kwa ibada, inayoambatana na njia ya msalaba katika kukumbuka mateso ya Yesu. Pia inaambatana na kusoma mistari ya Biblia, inayoeleza undani wa matukio yaliyosababisha kusulubiwa kwa Yesu Kristu.
Hii ni siku ambayo inatajwa kuwa na maana kubwa sana katika imani ya Kikristu......waumini wanaamini kwamba; kusulubiwa na kufa kwa Yesu kumeleta ukombozi duniani.

- Ijumaa Kuu haithibitishwi tu na vitabu vya dini, bali hata machapisho ya kihistoria yanathibitisha juu ya kusulubiwa na kufa kwa Yesu Kristu.

- Nami nasema; nawatakieni Ijumaa Kuu njema sana kwenu ninyi nyote!

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ijumaa kuu njema nawe pia na ahsante kwa neno la leo!!

Baraka Chibiriti said...

Asante sana Dada Yasinta!

WATEMBELEAJI