Tuesday, April 10, 2012

LALA SALAMA STEVEN KANUMBA!


Uendelevu wa Mwanadamu aliyezaliwa na Mwanamke na kuubwa kwa udongo, hutegemea sana pumzi na uhai kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ingawa Mwanadamu huwekwa katika kundi la wanyama, lakini huesabiwa kama mnyama mwenye akili kuliko wote. Ila kuna baadhi ya mambo kwake huwa ni giza..........watu wengi tulishawahi kujiuliza; kwanini hatuijui kesho wakati tuna Kalenda majumbani kwetu? au ulishawahi kuwaza ni kwanini hatuijui kesho yetu? Na mara nyingine ulishawahi kujiuliza pindi utakapo lala huelekea wapi? Hakuna ambaye ana jibu sahihi......haswa swali zito kwetu ni kuwa si kulala tu! ila mara nyingine huwa tunajiuliza kwanini tunakufa? Tunakwenda wapi baada ya kufa? na kipi kitakacho sababisha kifo chetu? Ingawa ni matamanio ya kila Binadamu, kutamani kufahamu hata tarehe, muda na wakati ambao Israeli atakuja kukatisha maisha yetu!

Basi tujitahidi sana kuwa tayari wakati wowote ule, tujitahidi sana kuwa wema daima na kuwajali wenzetu, pia kusali daima kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai anaotupatia, maana hatujui kabisa wakati wetu utakuwa lini.

Kwakweli kifo cha Kanumba kimetusikitisha sana sote, pole sana kwa ndugu na jamaa wote.....ila hatuna budi kumwombea ili Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani......Amina!

No comments:

WATEMBELEAJI