Sunday, April 1, 2012

MANENO MAZURI YA JUMAPILI HII YA LEO YA MATAWI.

Hosana mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana! Hosana Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli; Hosana juu mbinguni.

Utukufu, sifa na heshima kwako....ewe Kristu Mfalme Mkombozi; ndiwe uliyeimbiwa Hosana tamu na watoto wadogo.

Inueni vichwa vyenu enyi malango, naam; viinueni enyi malango ya milele, Mfalme wa Utukufu apate kuingia.
Ni nani huyu Mfalme wa Utukufu? Bwana wa majeshi, yeye ndiye Mfalme wa Utukufu.
Hosana juu mbinguni......Mbarikiwa wewe uliyekuja na wingi wa rehema!



Kanisa linakaribia sasa adhimisho la Kipasaka. Dominika ya Matawi ndio mwanzo wa Juma Kuu, ambalo kilele chake ni adhimisho la kufa na kufufuka kwake Yesu Kristu.

No comments:

WATEMBELEAJI